Thursday, February 9, 2017

Gwajima Atema Cheche,Amtaka Makonda Amtaje Ridhiwani Kikwete Kwenye List Yake...!!!!


Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?

Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.
Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;
1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi
2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.
Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.
Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.
Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.
Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.
Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais Magufuli, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.
Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono
Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.
Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana
Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.
Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa
Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?
Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?
Gwajima: Mimi nlikuwa mkali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa na hakuna hatua zilizokuwa zinachukuliwa.
Gwajima: Kuna Kipindi Ridhiwani Kikwete aliwapeleka Mahakamani Dr. Slaa na Mch. Mtikila akitaka wakanushe habari kuhusu utajiri wake, hiyo kesi sijui iliishia wapi.
Gwajima: Nani anamtumia Makonda?
Gwajima: Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.
Gwajima: Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?
Gwajima: Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.
Gwajima: Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?
Gwajima: Namfahamu rais Magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (Msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote na watendaji wote wa Serikali. Naamin rais hajamtuma Makonda.
Gwajima: Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.
Gwajima: Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nlikuwa namba tia yeye namba 10. Alikuwa ananiangalia jicho baya sana. Mimi, Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tunamechi si angenikamata hapo?
*Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine. Walikuwa na jina B sasa wamebadilisha jina.
Pata Habari Hizi Kupitia Android Application ya Udaku Special Blog, Bonyeza Hapa Kuinstall

Wednesday, February 8, 2017

Post za Masanja mkandamizaji, Idriss Sultani na Mbasha baada ya orodha ya Makonda leo

on
Leo February 8 Paul Makonda ametoa list ya awamu ya pili ya watu kwenye sakata la dawa za kulevya ambapo baada ya kuitaja orodha hiyo, baadhi ya watu wamepost vitu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.
Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji  >>>>alipost picha ya watu walioganda nakuandika “RC Makonda aliposema, MCHUNGAJI WANGU, alafu akatulia kwa muda bila kutaja jina, kuna watu walishaita Ambulance”

Idriss Sultan: “Makonda aliposema Idd asingemalizia nilikuwa nshakufa MUBASHARAAAA..!!!!

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha: Alipost picha ya Helicopter na kuandika haya “Atatua na hii kituo cha kati ijumaa saa 5

Baada ya Zoazoa ya Wasanii Wanaotumia na kuuza madawa ya kulevya kuwa Kubwa,Kitale Akana Rasmi Jina Lake ya Kitale Rais wa Mateja..!!!


Mchekesheja Maarufu Kitale,Hii leo kupiti ukurasa wake wa kijamii wa instagram amefunguka juu ya kulikana lililokuwa jina lake la awali la kitale Rais wa Mateja.
Hii Hapa Post yake huko Instagram..!!!
Pata Habari Hizi Kupitia Android Application ya Udaku Sp

Mkutano wa Yusuf Manji na Waandishi: Nitamshitaki Makonda Kwa Kunichafulia Jina


Baada ya Jina la Manji kutajwa katika majini 65 yaliyotangazwa leo na Mkuu wa Mkoa Makonda, Yusuph Manji Ameongea na Waandishi wa Habari na Kusema Haya:


Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.

Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.

Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?

Manji: Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.

Manji: Kama unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji: Hivi ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji: Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji: Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakiwa namvunjia heshima.

Manji: Mimi nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na wamsearch pia.

Manji: Mimi sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Keaho au keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji: Mkuu wa mkoa kuna sehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana naye kama diwani wa mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais.

By Figganigga/Jamii Forums

Tuesday, February 7, 2017

MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA KUIBUKA NA KOMPYUTA KWA KILA HAKIMU ACHAPE NAKALA ZA HUKUMU MWENYEWE


Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini-picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
******
Katika kuendana na kasi ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga inatarajia kuanzisha mpango wa kuhakikisha kila hakimu anakuwa na komputa mpakato ili kila hakimu achape hukumu yake mwenyewe.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard Kibela wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya mahakama hiyo mjini Shinyanga.
Jaji Kibela alisema katika kuendana na kasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mahakama hiyo inataka kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zinazotolewa na mahakama hiyo kwa wakati ili wapate muda wa kufanya shughuli zingine za maendeleo ili kukuza uchumi wa nchi.
“Katika matumizi ya TEHAMA mahakama yetu ina mpango wa kila hakimu awe na kompyuta mpakato ili kila hakimu aweze kuchapa hukumu yake mwenyewe ili kuongeza kasi ya nakala za hukumu kutolewa ndani ya siku 21.
Katika hatua nyingine Jaji Kibela alisema katika kipindi cha mwaka 2016 mahakama hiyo iliamua jumla ya mashauri 392 yakiwa ni kati ya mashauri yaliyokuwa yamefunguliwa na yake yaliyobaki mwaka 2015 ambayo kwa ujumla yalikuwa mashauri 1087.
“Kesi nyingi zimerithiwa kutoka mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora kabla ya kuanzisha kanda hii mwaka 2015 na pia baadhi ya majaji wamekuwa na majukumu mengine ya kikazi nje ya kanda.
Naye Kaimu mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea mkoa wa Shinyanga Paul Kaunda alisema nakala za hukumu hazichapwi kwa wakati n ahata zikichapwa mahakimu wamekuwa wakitumia muda mrefu kuzifanyia uhakiki hivyo kuchelewesha azma na haki yam kata rufaa katika mahakama za juu.
Aidha alisema pia ucheleweshaji wa utoaji haki kwa wakati unasababishwa na mahakama kuwa na mahakimu wachache kukabiliana na mashuri yanayofunguliwa kila siku.
Kaunda alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kuwashikilia watuhumiwa kituoni kwa zaidi ya saa 24 tangu mtuhumiwa akamatwe.
“Kifungu cha 32 na 33 cha sharia ya mwenendo wa makosa ya jinai kinawataka polisi wawe wamemfikisha mahakamani mtuhumiwa wa makosa ya jinai ndani ya masaa 24 lakini cha ajabu mamlaka ya jeshi la polisi imekuwa ikifanya kinyume na matakwa ya sheeria kwa sababu wanazozijua wenyewe”,alisema.
Naye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliwataka baadhi ya watu wanaosema mahakama inaingiliwa na katika majukumu wapuuzwe.
“Mahakama zetu ziko huru,naombeni muwapuuze watu wanaosema kwamba mahakama zinaingiliwa,nawaomba pia majaji na mahakimu mtoe haki kwa wakati kwani tunataka Tanzania mpya yenye haki,sisi tunaposema hapa kazi tu,basi nyie semeni hapa haki tu”,alisema Nkurlu.

AY Afunguka kuhusu msanii mwenzake wa East Coast Team kutumia madawa ya kulevya

Wiki hii nzima habari iliyomake headline ni kuhusu ishu ya madawa ya kulevya ambapo wasanii mbalimbali pamoja na watu wengine wamefikishwa polisi na wengine mahakamani kutokana na madawa ya kulevya.

Baada ya kuibuka kwa swala hili tumekuja kugundua kua kumbe kuna wasanii wengi wamehusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya. Msanii AY alipoulizwa kuhusiana na mmoja wa wasanii ambao walikua wakiunda kundi la East Cost Team kua ni mtumiaji wa madawa ya kulevya alifunguka haya.. Unaweza tazama video nzima hapa chini

Mwanafunzi wa Sekondari Atiwa Mbaroni Akiwa na Kete 24 za Cocaine..!!!


Polisi mkoani Mbeya wametangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete 24 za cocaine eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.

Kamanda wa polisi mkoa, Dhahir Kidavashari amesema Jumanne hii kuwa polisi wamemkamata mwanafunzi huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali na kwamba upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.

Kukamatwa kwa kijana huyo kunatokea siku moja baada ya Rais John Magufuli kuunga mkono kazi ya Makonda huku akiwaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote wanaojihusisha na dawa za kulevya bila kujali huyu ni nani.

Kidavashari amesema kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa ikiendelea, lakini sasa imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unasambaza dawa hizo.

Kweli Kufa Kufaana,Ray C Aamua Kuja na Kmapeni Hii Wakati Wema na Wenzake Wakiwa Ndani Kwa Kuhusishwa na Madawa ya Kulevya..!!

MSANII wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama‘Ray C’ Kiuno Bila Mfupa, amejitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuweka video mtandaoni ikimuonesha mtu aliyepoteza maisha kwa madawa ya kulevya huku akiandika: “SAY NO TO DRUGS”
Aidha Ray C ambaye anatajwa kama nimhanga wa madawa hayo aliwahi kupewa huduma vituo mbalimbali vinavyotoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya ‘Sober House’ na baada ya muda anaonekana kurudia hali ya kudhoofu na kuwa kama mhanga wa madawa hayo.
Ray C amewahamasisha watu wengi kupitia video aliyoiweka katika mtandao na imewagusa Watanzania wengi kwa kuchangia maoni yao juu ya athari mbaya za madawa ya kulevya na sakata la linalonguruma kwa sasa nchini.

Maamuzi ya mahakama kuhusu wasanii wanaoshtakiwa kwa dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imetoa maamuzi kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi  watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani