Mwanafunzi wa Sekondari Atiwa Mbaroni Akiwa na Kete 24 za Cocaine..!!!
Polisi
mkoani Mbeya wametangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa
na kete 24 za cocaine eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.
Kamanda
wa polisi mkoa, Dhahir Kidavashari amesema Jumanne hii kuwa polisi
wamemkamata mwanafunzi huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali
na kwamba upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.
Kukamatwa
kwa kijana huyo kunatokea siku moja baada ya Rais John Magufuli kuunga
mkono kazi ya Makonda huku akiwaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na
usalama kuwashughulikia wote wanaojihusisha na dawa za kulevya bila
kujali huyu ni nani.
Kidavashari
amesema kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa ikiendelea, lakini
sasa imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa
mtandao unasambaza dawa hizo.
No comments:
Post a Comment