Kweli Kufa Kufaana,Ray C Aamua Kuja na Kmapeni Hii Wakati Wema na Wenzake Wakiwa Ndani Kwa Kuhusishwa na Madawa ya Kulevya..!!
MSANII wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama‘Ray C’ Kiuno Bila
Mfupa, amejitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwa kuweka video mtandaoni ikimuonesha mtu aliyepoteza maisha
kwa madawa ya kulevya huku akiandika: “SAY NO TO DRUGS”
Aidha Ray C ambaye anatajwa kama nimhanga wa madawa hayo aliwahi kupewa
huduma vituo mbalimbali vinavyotoa huduma kwa waathirika wa madawa ya
kulevya ‘Sober House’ na baada ya muda anaonekana kurudia hali ya
kudhoofu na kuwa kama mhanga wa madawa hayo.
Ray C amewahamasisha watu wengi kupitia video aliyoiweka katika mtandao
na imewagusa Watanzania wengi kwa kuchangia maoni yao juu ya athari
mbaya za madawa ya kulevya na sakata la linalonguruma kwa sasa nchini.

No comments:
Post a Comment